Bara Hindi
From Wikipedia
Bara Hindi ni eneo kubwa ya Asia upande wa kusini ya milima ya Himalaya lenye kilomita za mraba milioni 4.5. Inaingia ndani ya bahari Hindi kama rasi kubwa sana lenye umbo la pembetatu.
[edit] Nchi za Bara Hindi
Nchi zifuatazo ni sehemu za Bara Hindi:
[edit] Jiografia
Kijiografia kuna sehemu tatu za:
- maeneo ya Himalaya (kaskazini ya Uhindi na Pakistan, Nepal, Bhutan)
- rasi ya Uhindi
- maeneo ya visiwa vya Bahari Hindi (Sri Lanka, Maldivi)
Kijiolojia Bara Hindi si sehemu ya Asia. Inakaa juu ya Bamba la Uhindi ambalo ni bamba la gandunia lililokuwa kama kisiwa kikubwa ndani ya Bahari Hindi hadi kujisukuma dhidi ya Bamba la Asia takriban miaka milioni 10 iliyopita. Mshtuko wa mgongano huu ulisababisha kukunja kwa ganda la dunia na kutokea kwa nyororo za milima ya Himalaya.
Categories: Bara | Asia | Rasi za Asia