Carlos Saavedra Lamas
From Wikipedia
Carlos Saavedra Lamas (1 Novemba, 1878 – 5 Mei, 1959) alikuwa mwanasheria na mwanasiasa kutoka nchi ya Argentina. Alikuwa Waziri ya Mambo ya Nje kuanzia 1932 hadi 1938. Wakati ule alisaidia kukomesha Vita ya Chako. Mwaka wa 1936 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.