Erik Axel Karlfeldt
From Wikipedia
Erik Axel Karlfeldt (20 Julai, 1864 – 8 Aprili, 1931) alikuwa mwandishi na mshairi kutoka nchi ya Sweden. Hasa aliandika mashairi juu ya maisha ya nchi yake. Mwaka wa 1931 aliteuliwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi. Aliteuliwa baada ya kufa tu; alikuwa ameikataa mwaka wa 1918.