Frederick Robbins
From Wikipedia
Frederick Chapman Robbins (25 Agosti, 1916 – 4 Agosti, 2003) alikuwa daktari wa watoto kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza virusi visababishavyo magonjwa mbalimbali. Mwaka wa 1954, pamoja na John Enders na Thomas Weller alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.