Funchal
From Wikipedia
Funchal ni mji mkuu wa visiwa vya Madeira ikiwa kwenye kisiwa kikuu kinachoitwa Madeira pia. Ni pia makao makuu ya wilaya ya Funchal. Madeira ni funguvisiwa ya Kireno katika sehemu ya Kiafrika ya Atlantiki.-
Maana ya neno "funchal" ni "shamari" - kwa sababu shamari ilipatikana kwa wingi wakati Wareno walipofika kisiwani mara ya kwanza.
Mji una wakazi 45,000 ni zaidi ya lakhi moja pamoja na mitaa ya nje. Kuna chuo kikuu cha Universidade da Madeira. Funchal ilikua pamoja na utalii wa watu tajiri.
Wilaya ya Funchal pana visiwa vya Porto Santo, Ilhas Desertas na Ilhas Selvagens pamoja na Madeira yenyewe.