Lakhi
From Wikipedia
Lakhi (pia Laki) ni neno la asili ya Kihindi la kutaja namba ya 100,000.
Mji una wakazi lakhi tano au mia tano elf. Namba 650,000 inaweza kusomwa "lakhi sita na nusu". Neno limeingia katika Kiswahili kutokana na historia ndefu ya mawasiliano ya kibiashara kati ya Bara Hindi na pwani la Afrika ya Mashariki.