Isaac Bashevis Singer
From Wikipedia
Isaac Bashevis Singer (14 Julai, 1904 – 24 Julai, 1991) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Poland ambapo alizaliwa na jina Yitskhek Bashyevis Zinger . Mwaka wa 1935 alihamia Marekani. Hasa aliandika riwaya na insha kuhusu maisha ya Wayahudi katika karne ya 20. Aliziandika katika lugha ya Kiyiddish. Mwaka wa 1978 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.