Johannes Vilhelm Jensen
From Wikipedia
Johannes Vilhelm Jensen (20 Januari, 1873 – 25 Novemba, 1950) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Anajulikana hasa kwa riwaya yake "Safari Ndefu" (kwa Kidenmark Den lange rejse) iliyotolewa katika majuzuu sita miaka ya 1908-22. Mwaka wa 1944 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.