Julian Huxley
From Wikipedia
Sir Julian Sorell Huxley (22 Juni, 1887 – 14 Februari, 1975) alikuwa mwanabiolojia na mwandishi kutoka nchi ya Uingereza. Anajulikana hasa kwa maandishi yake ya kisayansi aliyojaribu kuyafanya yaeleweke na watu wengi wa kawaida. Pia alikuwa mkurugenzi wa kwanza wa UNESCO. Alipewa cheo cha Sir cha Uingereza mwaka wa 1958.
Huxley alizaliwa ndani ya familia maarufu. Kwa mfano, kaka yake ni mwandishi Aldous Huxley, na kaka mwingine ni mwanabiolojia Andrew Huxley, mshindi wa Tuzo ya Nobel; baba yake ni mwandishi na mhariri Leonard Huxley. Tena, babu yake aliyemzaa mamake ni mwanabiolojia T. H. Huxley, aliyefanya kazi na kumsaidia Charles Darwin.
[edit] Viungo vya nje
[edit] Insha
- "Transhumanism" katika: New Bottles for New Wine. London: Chatto & Windus, 1957.
- "The New Divination" katika: Essays of a Humanist. London: Chatto & Windus, 1964.
[edit] Marejeo
- Clark, Ronald, W. 1968. "The Huxleys". McGraw-Hill
- Huxley, J., 1957. "Transhumanism". Angalia kiungo cha insha hiyo huko juu.
- Huxley, J., 1970. Memories. George Allen & Unwin, London.
- Kevles, D. J., 1985. In The Name Of Eugenics. University of California Press.