Kumasi
From Wikipedia
Kumasi ni mji mkubwa wa pili nchini Ghana na mji mkuu wa Mkoa wa Ashanti. Tangu mwaka 1695 ilikuwa mji mkuu wa Ufalme wa Ashanti na Asantehene (mfalme wa Ashanti) anakalia hadi leo jumba lake mjini. Ndipo kilipo "kikalio cha dhahabu" cha Asantehene ambacho kinaaminiwa kimeteremshwa kutoka mbinguni.
Mwaka 2005 mji ulikuwa na wakazi 862.000. Umbali kutoka Accra ni 250 km. Kuna Chuo Kikuu cha Kwame Nkrumah cha Sayansi na Teknolojia.
Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan amezaliwa Kumasi.
[edit] Viungo vya nje
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Kumasi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Kumasi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |