Milima ya Lebanoni ndogo
From Wikipedia
Lebanoni ndogo (pia: Antilebanon) ni safu ya milima katika Lebanoni, Syria na Israel inayoelea sambamba na milima ya Lebanoni yenyewe upande wa mashariki. Kati ya safu hizi mbili ni bonda la Beka'a. Upande mwingine iko Dameski mji mkuu wa Syria.
Safu ya Lebanoni ndogo ina urefu wa km 150. Milima mikubwa ni Hermoni (kar.: جبل الشيخ jabal-ash-Shaikh) mwenye kimo cha m 2,814 juu ya UB na Ta'a Musa (2,669 m).
Mpaka wa Syria na Lebanoni hufuata sehemu za juu za Lebanoni ndogo.
Safu inazuia mawingu yanayobeba mvua kutoka Mediteranea kufika hadi eneo la Dameski.