Mkoa wa Lindi
From Wikipedia
Lindi ni jina la mji, wilaya na mkoa wa Tanzania Kusini-Mashariki.
Contents |
[edit] Eneo la Mkoa wa Lindi
Mkoa wa Lindi umepakana na mikoa ya Pwani, Mtwara, Ruvuma na Morogoro. Upande wa mashariki hupakana na Bahari Hindi. Mkoa huu umeanzishwa mwaka 1971 una eneo la 67,000 km². Karibu robo ya eneo lake au 18,000 km² ni sehemu ya hifadhi ya wanyama ya Selous.
Mkoa una wilaya sita za Lindi Mjini na Lindi Vijijini, Kilwa, Nachingwea, Liwale na Ruangwa.
Mito mikubwa ndiyo Lukuledi, Matando na Mavuji, yote yaelekea Bahari Hindi. Mwinuko huanza mwambaoni ukipanda hadi mita 500, hakuna milima mirefu sana.
[edit] Wakazi
Mwaka 2002 idadi ya wakazi ilikuwa 791,306. Karibu asilimia 90 kati hao ndio wakulima. Makabila makubwa zaidi ni hasa Wamwera halafu Wamachinga na Wamatumbi na Wangindo huko Kilwa.
Idadi ya wakazi wa wilaya ni (idadi katika mabano): Kilwa (171,850), Lindi Mjini (41,549), Lindi Vijijini (215,764), Liwale (75,546), Nachingwea (162,081), Ruangwa (124,516),
[edit] Hali ya hewa
Hali ya hewa ya Lindi ni ya joto mwaka wote ikiwa na wastani kati ya sentigredi 24,5 na 27. Mkoa hupokea kati ya 980 mm na 1200 mm za mvua kwa mwaka, hasa kati ya miezi ya Novemba na Mei.
[edit] Barabara na mawasiliano
Kuna barabara chache katika hali nzuri. Ndizo 155 km za barabara ya lami na 3567 km barabara za udongo, mara nyingi katika hali mbaya. Wakati wa mvua mara kwa mara njia ya kwenda Daressalaam imefungwa. Kuna matumaini ya kuboreka kwa mawasiliano na mji mkuu wa Daresalaam tangu kumalizika kwa daraja la Rufiji.
Pana kiwanja cha ndege Lindi, Nachingwea na Kilwa Masoko. Lindi na Kilwa Masoko kuna pia mabandari. Huduma za simu zipata maendeleo kiasi tangu kuanzishwa kwa simu za mkononi.
Utalii haujafikia umuhimu sana kutokana na matatizo ya mawasiliano magumu ingawa Lindi ina sehemu mbalimbali zenye uwezo wa kuwavuta watalii: Kilwa Kisiwani ndicho mji wa kihistoria wa pwani la Afrika ya Mashariki pamoja na magofu ya miji mingine ya Waswahili, Selous ni hifadhi kubwa kabisa katika Afrika, ufukoni wa mchanga ni wa kuvutia sana, nafasi za zamia majini ni tele.
Gesi imepatikana baharini karibu na kisiwa cha Songosongo imeleta matumaini ya maendeleo.
|
|
---|---|
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |