Mkoa wa Mtwara
From Wikipedia
Mtwara ni jina la mji na mkoa wa Tanzania.
Mkoa wa Mtwara ni kati ya mikoa 26 ya Tanzania. Uko katika pembe la kusini-mashariki kabisa la nchi. Umepakana na Mkoa wa Lindi upande wa kaskazini, Bahari Hindi kwa mashariki, Msumbiji katika kusini na Mkoa wa Ruvuma upande wa Magharibi. Mpaka wa kusini ni Mto Ruvuma.
Ukiwa na 16,720 km² Mtwara ni mkoa mdogo katika Tanzania pamoja na Kilimanjaro.
Contents |
[edit] Wakazi
Jumla kuna wakazi 1,128,523 (sensa 2002). Wanawake wanazidi wakiwa 53 ya wakazi wote kwa sababu wanaume wengi hutoka nje kutafuta kazi.
Kati ya makabila ya Mtwara ndio Wamakonde wanaojulikana zaidi kutokana na sanaa yao ya uchongaji wa ubao hasa mpingo.
[edit] Utawala
Kuna wilaya 5: Mtwara Mjini (pia huitwa "Mikindani"), Mtwara Vijijini, Masasi, Newala na Tandahimba. Ndani yao ndipo tarafa 21, kata 98 na vijiji 554.
[edit] Uchumi
Mtwara iko kati ya mikoa iliyobaki nyuma miaka mingi kutokana na ugumu wa mawasiliano na barabara isiyopitika kwa sehemu kubwa ya kila mwaka.
Historia ya Mtwara unakuja sambamba na kumbukumbu la jaribio la Waingereza la kuanzisha mradi mkubwa wa maendeleo katika eneo hili ulioshindikana kabisa. Kuanzia 1947 serikali ya kikoloni ilijenga bandari ya Mtwara pamoja na reli. Vilevile Mtwara mjini ulipangwa vizuri na kubwa. Sababu yake ilikuwa mpango wa kuanzisha kilimo cha mashamba makubwa kwa ajili ya karanga hasa zilizohitajika kwa ajili ya mahitaji ya Waingereza ya mafuta ya kupikia. Mradi huu ulishindikana kabisa, pesa nyingi ilipotea hadi mradi ulifutwa kabla ya Tanzania kupata uhuru. Reli imeondolewa tena 1963.
Bandari imebaki ambayo haijaona kazi nyingi lakini bado ina faida ya kuwa na nafasi nzuri sana ya kupokea meli kubwa. Wakati wa mapambano dhidi ya serikali ya ubaguzi wa rangi katika Afrika Kusini mipango mbalimbali imetungwa kutengeneza njia ya kupeleka bishaa kutoka bandari ya Mtwara kwenda Songea na kutoka huko Malawi kwa kuvuka Ziwa la Nyasa.
Baada ya kujengwa kwa daraja mtoni Rufiji mwaka 2002 kuna matumaini mpya ya kuwa na barabara inayotumika kati ya Mtwara na Daressalaam. Eneo la Mnazi Bay ina gesi inayoweza kutumika kwa mahitaji ya nishati ya eneo lote.
[edit] Viungo vya nje
- Mtwara Region Homepage for the 2002 Tanzania National Census
- Tanzanian Government Directory Database
- [1]
|
|
---|---|
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |