Mlango wa Dover
From Wikipedia
Mlango wa Dover (Kifaransa: Pas de Calais; Kiing.: Strait of Dover) ni sehemu nyembamba ya Mfereji wa Kiingereza kati ya Ufaransa na Uingereza. Bahari ina upana wa 34 km pekee.
Kimataifa imekuwa kawaida kuuita kwa jina la mji wa Dover upande wa Uingereza. Wafaransa wanauita kufuatana na mji wa Calais uliopo upande wao wa mlango wa bahari.
Feri zinavuka kati ya miji ya Dover na Calais.