Mfereji wa Kiingereza
From Wikipedia
Mfereji wa Kiingereza ni mlango wa bahari kati ya Uingereza na Ufaransa. Urefu wake ni 560 km na sehemu nyembamba ni mlango wa Dover mwenye upana wa 34 km. Unaunganisha Bahari ya Kaskazini na Atlantiki upande wa kusini ya Britania.
[edit] Njia za kuvuka
Kwa karne nyini njia ya kuvuka mlango huu wa bahari ilikuwa safari kwa feri kati ya miji ya Calais (Ufaransa) na Dover (Uingereza). Tangu 1994 kuna handaki ya reli chini ya bahari. Reli inabeba abiria, motokaa zao na mizigo ya kila aina.
[edit] Mfereji wa Kiingereza kazika Historia
Maji kati ya kisiwa na Ulaya bara yalikuwa ulinzi wa Uingereza kwa muda wote wa historia yake. Ni mara chache tu ya kwamba wavamizi walifaulu kuvuka mfereji na kuingia.
Shambulizi la kwanza linalokumbukwa lilikuwa lile la Julius Caesar mnamo mwaka 55 KK. Waroma wa kale walifaulu kufanya Uingereza kuwa jimbo la Dola la Roma. Walipoondoka makabila ya Kigermanik kutoka Ujerumani na Skandinavia yaliingia kisiwani kwa kufika kwa vikundi vidogovidogo.
Shambulio la mwisho lililofaulu lilikuwa uvamamizi wa Wanormandy mwaka 1066.
Mipango yote ya baadaye ilishindikana: Wahispania mwaka 1588, Napoleoni mwanzo wa karne ya 19 na Hitler wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.