Pamanzi
From Wikipedia
Pamanzi (Kifaransa: Petite-Terre) ni kisiwa kidogo cha eneo la ng’ambo la Ufaransa la Mayotte. Kisiwa cha pili na kikubwa ni Mahore (Kifaransa: Grande-Terre).
Pamanzi ina eneo la 11 km². Mji mkubwa ni Dzaoudzi penye kiwanja cha ndege.
Kijiografia kisiwa ni sehemu ya funguvisiwa ya Komoro.