Mahore
From Wikipedia
Mahore (Kifaransa: Grande-Terre) ni kisiwa kikubwa cha eneo la ng’ambo la Ufaransa la Mayotte. Kisiwa cha pili ni Pamanzi (Kifaransa: Petite-Terre).
Mahore ina urefu wa 39 km na upana wa 22 km. Milima yake ni Mont Benara (660 m), Mont Choungui (594 m), Mont Mtsapere (572 m) et Mont Combani (477).
Mji mkubwa ni Mamoudzou. Kitovu cha kiuchumi ni Kawéni.
Kijiografia kisiwa ni sehemu ya funguviwa ya Komoro.