Pithagoras
From Wikipedia
Pithagoras (mwaka 580 mpaka mwaka 500 KK, hivi, Kigiriki: Πυθαγόρας), alikuwa mwanahisabati na mwanafalsafa Mwionia (Mgiriki), aliyeanzisha chama chenye siri kuhusu dini na sayansi kilichoitwa Pithagoreans, na kinachojulikana hasa kwa uhakiki “Pythagorean” ambao ulipewa jina lake.
Pithagoras ambaye huitwa “baba wa namba” alichangia hasa kwenye ualimu wa falsafa na dini wakati wa mwisho wa karne ya sita KK. Kwa sababu hekaya na mafumbo yanaficha kazi yake zaidi kuliko wengine walioishi kabla ya Sokrates, huwezi kuwa na uhakika kuhusu maisha na mafunzo yake. Pithagoras na wanafunzi wake waliamini kwamba kila kitu kinahusika hesabu, na walidhani kwamba inawezekana kutabiri na kupima kila kitu kwenye vielelezo au mizunguko yenye mahadhi.