Pyotr Kapitsa
From Wikipedia
Pyotr Leonidovich Kapitsa (8 Julai, 1894 – 8 Aprili, 1984) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Urusi. Hasa alichunguza nadharia ya usumaku. Alifanya kazi nchini Uingereza pamoja na Ernest Rutherford kuanzia mwaka wa 1921 hadi 1934 alipolazimishwa na Yosip Stalin kubaki Urusi kama mkurugenzi wa utafiti wa fizikia. Mwaka wa 1978, pamoja na Arno Penzias na Robert Woodrow Wilson alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.