Tufani
From Wikipedia
Tufani ni dhoruba kali inayoanza juu ya bahari katika maeneo ya tropiki yenye upepo mwenye kasi ya zaidi ya 117 km/h.
Inaanza juu ya bahari ya kitropiki penye maji yenye halijoto juu ya 26 °C. Hewa joto yenye mvuke nyingi iananza kupanda juu na kuzunguka. Mzunguko huo unaongezeka kasi kuwa dhoruba. Kasi ikifikia mwendo wa 117 km/h inaitwa tufani.
Tufani zinatokea katika bahari zote penye maji ya moto kaskazini na kusini ya ikweta.
[edit] Hatari za tufani
Tufani inaweza kusababisha hasara kubwa ikigusa meli baharini na zaidi mwambaoni inapofikia nchi kavu au visiwa.
Hatari zake ni hasa kasi ya upepo pamoja na kiasi kikubwa cha mvua. Kasi ya upepo inaweza kurusha vitu vizito kama miti, paa za nyumba au magari na kuvirusha mbali. Watu huuawa na mali kuharibiwa. Uwingi wa mvua husababisha mifuriko.
[edit] Majina ya tufani
Atlantiki kwa mfano inaona takriban tufani kumi au zaidi kila mwaka. Zinapewa majina kufuatana alfabeti. Imekuwa kawaida tangu 1979 kutumia majina ya kiume na ya kike kwa kubadilishana (zamani zilipewa majina ya kike tu lakini wanawake walilalamika).
Wataalamu wanatumia orodha sita ya majina hivyo jina linaweza kurudia baada ya miaka sita.
Tufani ya "Katrina" iliyoharibu mji wa New Orleans katika Agosti 2005 ilikuwa tufani ya 11 ya mwaka 2005. Ilifuata tufani "Jose" na kufuatwa na "Lee" halafu "Maria". Kama tufani inasababisha uharibifu mkubwa sana jina lake huondolewa katika orodha maana yake jina hili halitarudia. "Katrina" imebadilishwa kwa "Katia" katika orodha ya mwaka itakayotumika mwaka 2011 (ikitokea itakuwa tufani baada ya "Jose" ya 2011)
Katika kila bahari kuna utaratibu wa pekee wa kutolea majina.