Wilaya ya Kilwa
From Wikipedia
Wilaya ya Kilwa iko katika Mkoa wa Lindi, takriban kilometa 220 kusini mwa Dar es salaam. Kilwa imepakana na Mkoa wa Pwani upande wa kaskazini, Bahari ya Hindi upande wa mashariki, wilaya ya Lindi Vijijini upande wa kusini na wilaya ya Liwale upande wa magharibi. Kuna wakazi 171,850.
Makao makuu ya wilaya ni Kilwa Masoko.
Wilaya hii ina tarafa/shehia zifuatazo (idadi ya wakazi 2002 katika mabano): Tingi (5,823), Miteja (5,568), Mingumbi (10,543), Kijumbi (12,576), Chumo (16,809), Kipatimu (23,007), Kandawale (5,018), Njinjo (5,942), Mitole (3,559), Miguruwe (2,589), Likawage (3,426), Nanjirinji (5,535), Kiranjeranje (7,597), Mandawa (10,839), Lihimalyao (8,824), Pande (11,645), Kikole (4,275), Kivinje Singino (13,374), Songosongo (2,577), Masoko (12,324)