Yohane IV
From Wikipedia
Yohannes IV (* 1831 kwa jina la Dejazmach Kassay; † 10 Machi 1889 Metemma, Sudan) alikuwa Ras wa Tigray na Kaisari wa Ethiopia kati ya 1872–1889. Alimfuata Tewodros II akifaulu kutawala juu ya majimbo yote ya Ethiopia.
1876 aliweza kuzuia mashambulio ya Misri dhidi ya Ethiopia.
Aliuawa katika mapigano ya Metemna dhidi ya jeshi la Al-Mahdi tar. 10 Machi 1889. Kichwa chake kilikatwa na kuonyeshwa baadaye Omdurman.