André Gide
From Wikipedia
André Gide (22 Novemba, 1869 – 19 Februari, 1951) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Ufaransa. Mada za maandiko yake ni pamoja na kumtafuta Mungu, shajara za maisha yake, na ushoga. Tawasifu yake "Punje ya Ngano Isipokufa ..." (kwa Kifaransa Si le grain ne meurt ...) ilitolewa mwaka wa 1926. Mwaka wa 1947 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.