Bendera ya Guinea
From Wikipedia
Bendera ya Guinea ina milia mitatu ya kusimama yenye rangi za nyekundu, njano na kijani - kibichi. Rangi hizi ziko pia kwenye bendera ya Ethiopia na ya Ghana zinaonyesha athira za Ethiopia (nchi ya Afrika iliyofaulu kujitetea dhidi ya ukoloni) na pia Ghana (nchi ya kwanza ya Afrika ya kupata uhuru baada ya ukoloni).
Mara nyingi rangi hizi huelezwa kuwa na maana kama ifuatayo:
- nyekundu kuwa rangi ya damu iliyomwagika katika mapambano ya kufikia uhuru
- njano ni jua, mwanga wa juu na pia utajiri wa dhahabu ya Guinea
- kijani ni rangi ya nchi, ya kilimo na mimea na ya maendeleo kwa kazi ya wakulima
Waguinea wamependa kuzilinganisha na maneno ya wito la tauifa: Travail, Justice, Solidarité (kazi, haki, kushikamana)