Dublin
From Wikipedia
Dublin (Kieire pia: Baile Ãtha Cliath = "Kijiji kwenye kivuko kwa mafunjo") ni mji mkuu wa Jamhuri ya Eire pia mji mkuu kwenye kisiwa cha Eire mwenye wakazi milioni 1.6 kwenye rundiko la jiji.
Contents[Ficha] |
[edit] Jiografia
Dublin iko kando la mdomo wa mto Liffey unapoishia katika Atlantiki kwenye pwani la mashariki la Eire.
[edit] Historia
Wataalamu kadhaa hujaribu kuona uhusiano kati ya mji wa "Ebalana" uliotajwa na katika maandiko ya Ptolemeo mnamo 140 BK lakini hakuna uhakika kuhusu mahali pake.
Mji wa leo ulianzishwa kama kiji cha wavuvi kwa jina la „Ãth Cliath“ na kando lake Wavikingi walijenga kijiji cha jirani cha „Dubh Linn“ ("matope mweusi"). Vijiji vikaungana na kuwa mji tangu 1172 kwa sababu Wanormandi baada ya kuvamia Eire kutoka Uingereza walianzisha makao makuu yao hapa. Katika kipindi hadi karne ya 16 Dublin ilikuwa kitovu cha eneo lililokuwa chini ya wafalme wa Uingereza kisiwani na tangu 1541 mji mkuu wa Ufalme wa Eire uliotawaliwa na mfalme wa Uingereza.
Baada ya maungano wa Uingereza na Eire katika Ufalme wa Maungano Dublin ilikuwa makao ya gavana mwingereza.
Uhuru wa Eire ulianza 1916 mjini Dublin kwenye uasi wa Pasaka. Kwenye Vita ya Uhuru ya Eire nyumba nyingi ziliharibiwa. Tangu uhuru wa 1922 Dublin ikawa mji mkuu.
Baada ya kujiunga kwa Eire na Umoja wa Ulaya Dublin imeendelea kukua na kuwa jiji ya Kiulaya. 1998 Dublin ilisheherekea sikukuu ya kumaliza miaka 1000.
[edit] Viungo vya Nje
- "The Reflecting City"
- Dublin GDP stats
- WikiSatellite view of Dublin at WikiMapia
- The Dublin Community Blog
- Satellite map of Dublin - Including local geographic features.
[edit] Picha za Dublin
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Dublin" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Dublin kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |