Edward Muungamaji
From Wikipedia
Edward Muungamaji (takriban 1003 – 5 Januari, 1066) alikuwa mfalme wa Uingereza kuanzia mwaka wa 1042 hadi kifo chake. (Kwa Kiingereza huitwa Edward the Confessor.) Kama mfalme hakuwa na nguvu ya kutawala lakini maisha yake ya kikristo yalikuwa mfano mwema kabisa. Mwaka wa 1161 alitangazwa kuwa mtakatifu. Sikukuu yake ni 13 Oktoba.