Galapagos
From Wikipedia
Galapagos ni jina la funguvisiwa ya Ekuador katika Pasifiki takriban 1000 km kutoka pwani la bara ya Amerika Kusini. Jumla ya visiwa ni 61 kati ya hivi kuna 13 vikubwa. Visiwa vimesambaa katika eneo la 8000 km².
Funguvisiwa ni ya asili ya kivolkeno. Visiwa ni mashuhuri duniani kwa sababu ya idadi kubwa ya spishi za wanyama. Charles Darwin alifanya utafiti wa spishi nyingi akapata dhana za kimsingi kwa ajili ya nadharia yake ya mageuko ya spishi.
Visiwa vikubwa ni kama vifuatavyo:
- Santiago
- Santa Cruz
- Floreana
- San Cristobal
- Española*
- Genovesa
- Santa Fe
- Isabela*
- Fernandina
- Darwin
- Roca Redonda
- Marchena
- Pinta
[edit] Viungo vya Nje
- Galápagos Islands xeric scrub (World Wildlife Fund)
- Galápagos geology - the page also includes much general information on the Galápagos Islands