Guadeloupe
From Wikipedia
Guadeloupe ni eneo la ng'ambo na mkoa (departement)wa Ufaransa katika Bahari ya Karibi lenye visiwa tisa vidogo. Mji mkuu ni Basse-Terre.
Wakazi asilia walikuwa Waindio. Utamaduni wao uliharibiwa kabisa kwa kuja kwa ukoloni wa Ulaya. Ikawa koloni ya Ufaransa halafu ya Uingereza halafu ya Uswidi halafu ya Ufaransa tena.
Eneo lake ni 1,780 km². Idadi ya wakazi ni takriban lakhi 4 na nusu. Asilimia 90 za wakazi ni wa asili ya Kiafrika ikiwa wazee wao walipelekwa hapa kama watumwa kwa ajili ya kazi za mashamba ya miwa.
[edit] Tazama pia
- Martinique ni eneo nyingine ya Ufaransa katika Bahari ya Karibi.