Kofi Annan
From Wikipedia
Kofi Annan alikuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa 1996 - 2006. Alizaliwa 8 Aprili 1938 huko Kumasi, Ghana. Alipewa jina Kofi kuonyesha kuwa alizaliwa siku ya Ijumaa kuendana na utamaduni wa Ashanti. Jina Annan linamaanisha kuwa alikuwa ni mtoto wa nne kuzaliwa.
Baada ya masomo ya uchumi alijiunga na huduma ya Umoja wa Mataifa mwaka 1962 katika WHO. 1974-1976 alifanya kazi Ghana halafu akarudi tena huduma ya UM. Akapanda ngazi kuwa Makamu wa Katibu Mkuu mhusika wa usalama aliwajibika kusimamia shughuli za wanajeshi walio chini ya UM.
Alihusika na vita ya Rwanda pia ya Yugoslavia ambako wanajeshi chini ya bendera ya UM walishirikiana.
1996 alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa UM, akarudishwa cheo mwaka 2001.
Kofi Annan ameoa mara ya pili. Mke wake Nane Maria Annan anatoka Uswidi. Ana watoto watatu.