Makka
From Wikipedia
Makka (rasmi: Makkah al-Mukarramah; Kar.: مكة المكرمة) ni mji wa Ufalme wa Uarabuni wa Saudia. Ina wakazi 1,294,167 (mwaka 2004). Mji uko kwenye bonde la Ibrahimu mnamo km 80 kutoka pwani la Bahari ya Shamu na bandari ya Jeddah. Mazingira ya mji ni jangwa mahali penyewe kuna visima vilivyowezesha kuwepo kwa mji tangu kale.
[edit] Makka kama mahali patakatifu wa Uislamu
Makka ni mji mtakatifu wa Uislamu. Kila mwaka mamilioni wa Waislamu wanahiji kwenda Makka. Wakati huu wa hajj wanajaribu kufuata nyayo za mtume Muhammad. Makka ni mji uliofungwa kwa wasio Waislamu.
Kwa Waislamu Makka ni mji wa kuzaliwa kwake mtume Muhammad pia mahali alipokaa alipoanza kupokea aya za Kurani. Mjini kuna pia jengo la Kaaba linaloaminiwa ni msikiti iliyojengwa na Adamu na kutengenezwa upya na Ibrahimu (Abrahamu).
Hajj ya kwenda Makka ni moja kati ya nguzo tano za Uislamu.
Makka mwaka 1850 |
|||
[edit] Tovuti za Nje
Makala hiyo kuhusu "Makka" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Makka kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |