Max von Laue
From Wikipedia
Max von Laue (9 Oktoba, 1879 – 24 Aprili, 1960) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ujerumani. Pamoja na utafiti mwingine alichunguza mionzi ya eksirei. Mwaka wa 1914 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Tangu mwaka wa 1950 alikuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Max Planck kwa kemia ya kifizikia kule Berlin.