May Ayim
From Wikipedia
May Ayim (3 Mei, 1960 – 9 Agosti, 1996) alikuwa mwandishi wa kike kutoka nchi ya Ujerumani. Baba yake ni Mghana na mama yake Mjerumani. Alilelewa mbali na wazazi wake na familia waliompanga chini ya jina la May Opitz. Alijihusisha hasa na haki za Waafrika nchini Ujerumani. Alipotambuliwa kuwa na ugonjwa wa kukacha kwa seli (kwa Kiingereza multiple sclerosis) alikata tamaa na kujiua.
Tangu mwaka wa 2004, shirika la UNESCO hutoa Tuzo ya May Ayim kwa ajili ya fasihi ya Kijerumani iliyoandikwa na Waafrika.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "May Ayim" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu May Ayim kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |