Mbuni
From Wikipedia
Mbuni | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mbuni Somali
|
||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Mbuni ni ndege wa familia Struthionidae. Kuna spishi mbili kwa jenasi moja, lakini wataalamu wengine wanafikiri ni spishi moja tu. Ndege hawa ni wakubwa kuliko wengine wote. Wana miguu mirefu na shingo refu na wanaweza kukimbia sana, hata kwa mwendo wa 65 km kwa saa, lakini hawawezi kuruka angani. Mbuni wanaishi savana na nyika na majangwa za Afrika, lakini wanafugwa ulimwengu wote. Jina la sayansi la spishi kuu, Struthio camelus, linatoka lugha ya Kiyunani: στρουθιον = jurawa na καμηλος = ngamia.
[edit] Spishi
- Struthio camelus, Mbuni Kawaida (Common Ostrich)
- S. c. australis, Mbuni Kusi in (South African Ostrich): shingo na miguu ya dume buluu kidogo.
- S. c. camelus, Mbuni Kaskazi (North African Ostrich): shingo ya dume nyekundu.
- S. c. massaicus, Mbuni Masai (Masai Ostrich): shingo na miguu ya dume pinki.
- S. c. syriacus, Mbuni Arabu (Arabian ostrich): imekwisha sasa
- S. molybdophanes, Mbuni Somali (Somali Ostrich): shingo na miguu ya dume buluu.