Nyota
From Wikipedia
Nyota ni gimba kubwa angani linalong'aa kwa sababu inatoa mwanga, joto na aina mbalimbali za mnururisho kutokana na myeyungano ya kinyukilia ndani yake. Jua letu ni nyota iliyo karibu na sayari yetu ya dunia tunapoishi. Kutokana na joto kali mada yake ni katika hali ya utegili yaani kama gesi ya joto sana.
Kwa macho haiwezekani kutofautisha mara moja nyota na sayari. Kwa hiyo katika lugha ya kila siku sayari huitwa mara nyingi "nyota" ikionekana kwa macho.
Habari za nyota zinakusanywa na kunfanyiwa utafiti na sayansi ya falaki. Kuna pia elimu ya unajimu ambayo ni elimu ya karne nyingi lakini haifuati utaratibu wa kisayansi ikijaribu kutabiri kutokana na nyota.
[edit] Idadi ya nyota
Nyota zinazoonekana kwa macho wakati wa usiku ni kama 6000 lakini idadi yao hali halisi ni kubwa zaidi. Hakuna aliyeweza kuhesabu nyota zotelakini kuna makadirio ya kuwa idadi inaweza kufika 70,000,000,000,000,000,000,000.
[edit] Galaksi
Nyota hupatikana angani katika makundi kama mawingu makubwa sana. Kundi kama hili huitwa galaksi. Galaksi yetu ikiwemo mfumo wa jua letu imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000.
[edit] Umbali kati ya nyota
Kutokana na umbali mkubwa kati ya nyota na nyota umbali huu hutajwa kwa kipimo cha mwaka wa nuru. Nyota jirani kabisa na jua letu inaitwa Alpha Centauri umbali wake ni 4.2 miaka ya nuru maana yake nuru yake inahitaji zaidi ya miaka minne hadi imefika kwetu. Kwa maana nyingine tunaiona nyota hii jinsi ilivyoonekana miaka minne iliyopita.
Galaksi ya jirani inayoitwa Andromeda ina umbali wa miaka ya nuru milioni 2.5. Maana yake mwanga wake unahitajia miaka milioni mbili na nusu mpaka kuonekana kwetu au kwa lugha nyingine tunaona galaksi ya Andromeda jinsi ilivyoonekana miaka hii milioni mbli na nusu iliyopita.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Nyota" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Nyota kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |