Tanganyika (nchi)
From Wikipedia
Tanganyika ni jina la kihistoria kwa ajili ya Tanzania bara pamoja na visiwa vya Mafia na Kilwa.
[edit] Koloni ya Kiingereza baada ya kuondoka kwa Wajerumani
Jina hili limekuwa kawaida baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia wakati Uingereza ulipata utawala juu ya nchi.
Tanganyika ilikuwa sehemu kubwa ya koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kasoro maeneo ya Rwanda na Burundi.
Tanganyika imekabidhiwa kwa Uingereza na Shirikisho la Mataifa 1920 baada ya vita vikuu ya kwanza wakati Ujerumani imepotea koloni zake zote.
Waingerezea waliamua kutumia jina ya Tanganyika kwa ajili ya eneo hili kutokana na ziwa kubwa ambalo ni mpaka wa mashariki wa eneo lake.
[edit] Uhuru na Maungano na Zanzibar
Tanganyika imepata uhuru wake tar. 09.12.1961 (taz.: Historia ya Tanzania).
Mwaka 1964 imeunganishwa na Zanzibar kuwa Jamhuri ya Maungano ya Tanzania.
Leo hii neno "Tanganyika" latumiwa wakati mwingine kutaja sehemu ya Tanzania isiyo Zanzibar.