Tarso
From Wikipedia
Tarso [[(Kituruki na Kilatini: Tarsus; Kigiriki: Ταρσός)]]- ni mji wa kale katika wilaya ya Mersin ya Uturuki ya Kusini. Iko mdomoni wa mto Tarsus Cay (jina la kale: Kydnos) karibu na mwambao wa Mediteranea. Mji una wakazi 216,382 (sensa ya mwaka 2000).
[edit] Mji wa Mtume Paulo
Tarso au Tarsus imejulikana zaidi kama mji alikozaliwa mtume wa Kikristo Paulo wa Tarso. Mji ulianzishwa tayari katika milenia ya nne KK. Tarso ilikuwa na majina mbalimbali katika historia yake kama vile Antiokia kwa Kydnos au Juliopolis. Tangu karne ya kwanza KK mji ulikuwa chini ya Dola la Roma. Wakazi wake wote pamoja na Wayahudi wa mji walipewa uraia wa Kiroma. Hivyo Paulo alikuwa raia Mroma.