Tehran
From Wikipedia
Tehran (au Teheran - تهران kwa Kifarsi) ni mji mkuu wa Uajemi. Idadi ya wakazi inakadiriwa kuwa kati ya milioni 7 hadi 12.
Tehran ilichukua nafasi ya mji wa Ray mji mkuu wa kale ulioharibiwa mwaka 1220 na Wamongolia.
Siku hizi mji umeenea kwenye mtelemko wa milima ya Elburs kwenye kimo kati ya mita 1000 hadi 1700 juu ya UB. Kwa jumla mitaa maskini zaidi iko kusini ya mji katika tambarare ya jangwa la Dasht-e-kavir. Mitaa tajiri iko upande wa kaskazini kwenye mitelemko ya milima.
Makala hiyo kuhusu "Tehran" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Tehran kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Categories: Mbegu | Miji Mikuu Asia | Miji ya Uajemi | Uajemi | Tehran