Ulaya ya Kazkazini
From Wikipedia

Ulaya ya Kaskazini ni sehemu ya kaskazini ya bara la Ulaya. Kuna maelezo ya kutofautiana ni nchi zipi ambazo ni sehemu ya kanda hili.
Kwa hakika tamko hili lamaanisha:
- Nchi za Skandinavia pamoja na Denmark, Ufini, Iceland, Norwei na Uswidi, pia visiwa vya Faroe.
- Nchi za Kibalti yaani Estonia, Latvia na Lithuania.
- Mara nyingi ama sehemu ya kaskazini ya Britania (=Uskoti) au funguvisiwa ya Britania yote huhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya ya kaskazini yaani Uingereza, Uskoti, Welisi, Ueire na kisiwa cha Man.
- Wakati mwingine hata nchi nyingine kando la Bahari ya Baltiki kama Urusi ya kaskazini-magharibi, Poland ya kaskazini, Ujerumani ya Kaskazini zinahesabiwa humo.