Visiwa vya Cook
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: Te Atua Mou E Mungu ni Ukweli |
|||||
Mji mkuu | Avarua |
||||
Mji mkubwa nchini | Avarua | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza Kimaori |
||||
Serikali | Template:Nowrap Elizabeth II wa Uingereza Sir Frederick Goodwin Jim Marurai |
||||
Uhuru Kujitawala kwa ushirikano wa hiari na New Zealand |
4 Agosti 1965 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
236 km² (ya 209) -- |
||||
Idadi ya watu - Mar 2006 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
18,700 (ya 218 (2005)) 18,027 76/km² (ya 117) |
||||
Fedha | Dollar ya New Zealand (pia Dollar ya Cook Islands) ( NZD ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-10) (UTC) |
||||
Intaneti TLD | .ck | ||||
Kodi ya simu | +682 |
Visiwa vya Cook (Kimaori: Kūki 'Āirani) ni nchi huru ya Polynesia katika Pasifiki iliyopo katika hali ya ushirikiano wa hiari na New Zealand. Eneo lake ni visiwa vidogo 15 vyenye eneo la 240 km². Mji mkuu wa Avarua uko kwenye kisiwa cha Rarotonga.
Visiwa vilikuwa eneo lindwa la Uingereza katika karne ya 19 kufuatana na ombi la malkia wa Cook aliyeogopa uvamizi wa Ufaransa wakati ule. Chini ya utawala wa Kiingereza viliwekwa chini ya usimamizi wa serikali ya New Zealand zikabaki hivyo katika hatua mbalimbali za uhuru wa New Zealand. 1965 New Zealand ikawapa watu wa Cook nafasi ya kujiamulia kuhusu uhuru wao. Visiwa viliamua kujitawala katika ushirikiano na New Zealand. Hatua hii ilisimamiwa na Umoja wa Mataifa kwa azimio lake No. 1514 (XV).
Sheria huamuliwa na bunge la visiwa vya Cook. Serikali haisimamiwi na New Zealand. Wananchi wote wanashika uraia wa New Zealand inaoendesha pia shughuli za jeshi na siasa ya nje kwa niaba ya visiwa. Visiwa vya Cokk vimebaki na nafasi kufanya mapatano yao na nchi za nje vilevile.
Utalii ni bisahara kuu visiwani.