Elizabeth II wa Uingereza
From Wikipedia
Elisabeth II ni malkia wa Uingereza (au Ufalme wa Maungano) tangu 1952. Alizaliwa kwa jina la Elizabeth Alexandra Mary Windsor tar. 21 Aprili 1926 mjini London kama mtoto wa kwanza wa mfalme Georg VI na Elizabeth Bowes-Lyon.
Kama mkuu wa Jumuiya ya Madola yeye ni pia mkuu wa dola wa nchi zifuatazo n´dani ya jumuiya hii:
- Malkia wa Antigua na Barbuda
- Malkia wa Australia
- Malkia wa Bahamas
- Malkia wa Barbados
- Malkia wa Belize
- Malkia wa Kanada
- Malkia wa Grenada
- Malkia wa Jamaika
- Malkia wa New Zealand
- Malkia wa Papua Guinea Mpya
- Malkia wa Saint Kitts na Nevis
- Malkia wa Saint Lucia
- Malkia wa Saint Vincent na Grenadini
- Malkia wa the Visiwa vya Solomon
- Malkia wa Tuvalu
- Malkia wa Ufalme wa Maungano ya Britania na Eire ya Kaskazini
Alitangazwa kuwa malkia tar. 6 Februari 1952 mara moja baada ya kifo cha babake George VI. Wakati ule alikuwa akitembelea Kenya iliyokuwa bado koloni ya Uingereza akatembelea milima ya Aberdares.
Alipokea taji katika ibada rasmi tar. 2 Juni 1953 kwenye kanisa la Westminster Abbey.
Katika nchi zote anaposhika cheo hana mamlaka ya kiserikali anatawala kama mfalme wa kikatiba katika muundo wa serikali ya kibunge.