Abidjan
From Wikipedia
Abidjan ni mji mkubwa nchini Cote d'Ivoire pia ni mji mkuu hali halisi. Vilevile ni bandari kuu ya nchi kwenye Ghuba ya Guinea ya bahari ya Atlantiki. Abidjan haiko baharini moja kwa moja lakini kwenye wangwa ya Ebrie inayotengwa na bahari kwa kanda nyembamba ya mchanga.
Abidjan imekua haraka kuanzia wakazi 65,000 mwaka 1950 hadi wakazi 3,692,570 mwaka 2005. Ilikuwa pia mji mkuu rasmi kati ya 1934 hadi 1983.
Kuna viwanda vya ngozi, nguo, vyakula na mafuta.
Abidjan ilikuwa kijiji tu hadi mwaka 1904. Wakati ule iliteuliwa kuwa mwanzo wa reli ya kuelekea ndani. Reli ilianzishwa hapa kwa sababu ng'ambo ya wangwa ilikuwepo bandari ndogo ya Port-Bouët. Tangu reli kujengwa Abidjan ilikua haraka. Mwaka 1934 ilitangazwa kuwa mji mkuu wa koloni ya Kifaransa Cote d'Ivoire.
Mwaka 1950 mfereji wa Vridi ilikata kanda la mchanga na kufungua wangwa kwa meli kutoka bahari; wangwa ikawa bandari kubwa yenye usalama mzuri kwa meli, na Abidjan ikawa mji wa bandari iliyosababisha kukua kwa uchumi na kuongezeka kwa watu.
Abidjan kuna chuo kikuu tangu 1964.
Tangu mwanzo wa vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2004 hali ya usalama mjini umeshuka chini sana.