Ghuba ya Guinea
From Wikipedia
Ghuba ya Guinea ni kidaka kikubwa cha Atlantiki kwenye pwani la magharibi ya Afrika.
Eneo lake linahesabiwa kuanza nchini Liberia kwenye rasi ya Palmas na kwisha kwenye rasi Lopez nchini Gabon.
Jina la "Guinea" limetokana na jina la kale kwa ajili ya sehemu kubwa ya upande wa kusini ya Afrika ya Magharibi kati ya jangwa la Sahara na Atlantiki likimaanisha "nchi ya watu weusi" kwa lugha ya kiberber.
Kati ya mito mikubwa inayoishia kwenye ghuba ni Niger, Volta na Kongo. Mwambao wa ghuba ina vidaka viwili vidogo ni hori ya Benin na hori ya Biafra (Nigeria imebadilisha jina hili kuwa hori ya Bonny baada ya vita ya Biafra).