Alpha
From Wikipedia
Alfa (pia: alpha) ni herufi ya kwanza ya Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa kama Α (herufi kubwa cha mwanzo) au α (herufi ndogo ya kawaida).
Katika Ugiriki ya Kale ilihesabiwa pia kama namba "1".
Jinsi ilivyo kawaida na herufi mbalimbali za kigiriki inatumiwa kama kifupi kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na fisikia. Imejulikana hasa kama jina la pembe ya kwanza katika pembetatu.
Katika falaki inatumiwa kuanza hesabu ya nyota katika kundinyota. Kwa mfano nyota yetu jirani katika ulimwengu inaitwa "Alfa Centauri". Imeitwa hivyo kwa sababu inang'aa kushinda nyota zota za kundinyota ya Centaurus. Inayofuata ni "beta Centauri" na kadhalika.