Bogota
From Wikipedia
Bogota au kwa jina kamili Santa Fe de Bogotá ni mji mkuu wa Kolombia pia mji mkubwa wa nchi mwenye wakazi milioni saba takriban.
Mji uko katika nyanda za juu kwenye kimo cha 2,640 m juu ya UB kati ya milima ya Guadalupe (3,317 m) na Monserrate (3,100 m).
Mji ulianzishwa na Mhispania Gonzalo Jiménez de Quesada tar. 6 Agosti 1538 kwenye mahali pa soko la Wachibcha lililoitwa "Bacata". Quesada alitumia jina la "Santa Fe" (kihisp.: "imani takatifu") kutokana na mji wa Hispania alikotokea mwenyewe.
Baadaye mji uliongezewa jina la pili "Bogota" kutokana na jina asilia "Bacata". Jina kamili lilikuwa "Santa Fe de Bogota".
Makala hiyo kuhusu "Bogota" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Bogota kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |