Brasilia
From Wikipedia
Brasília ni mji mkuu wa Brazil mwenye wakazi 2,282,049. Ni mji mpya uliojengwa baada ya katika miaka 1956 - 1960 BK.
Mji mkuu ulihamishwa kutoka Rio de Janeiro uliyoko pwani na kandokando la eneo la Brazil kwenda mji mpya wa Brasilia kuanzia mwaka 1960. Brasilia ilijengwa mahali pasipo na mji kabla ya ujenzi wake. Ujenzi ulilenga kupata mji mkuu ulioko katikati ya nchi na kuachana na mapokeo ya kikoloni yaliyojenga mji mku mwambaoni wa bahari kwa sababu ya mawasiliano kati ya koloni na nchi tawala.
Brasilia iko kwenye nyanda ya juu katika kimo cha 1,000 m juu ya UB.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Brasilia" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Brasilia kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |