Edward Tatum
From Wikipedia
Edward Lawrie Tatum (14 Desemba, 1909 – 5 Novemba, 1975) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza uhusiano kati ya jeni na vimeng’enya. Mwaka wa 1958, pamoja na George Beadle na Joshua Lederberg alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.