Niger (mto)
From Wikipedia
Mto wa Niger | |
---|---|
|
|
Chanzo | Futa Djalon, Guinea |
Mdomo | Atlantiki |
Nchi za beseni ya mto | Guinea, Mali, Niger, Benin na Nigeria |
Urefu | 4,374 km |
Kimo cha chanzo | 800 m |
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni | 6,000 m³/s |
Eneo la beseni (km²) | 1,900,000 km² |
Niger ni mto mrefu wa tatu wa Afrika ikiwa na mwendo wa 4.374 km. Njia yake ni kama pinde ikianza Guinea katika nyanda za juu za Futa Djallon kuelekea kaskazini-mashariki kupitia Mali hadi Niger. Karibu na mji wa Timbuktu inageukia kuelekea mashariki, halafu mashariki-kusini kupitia Benin na Nigeria hadi kufika mdomoni wa delta yake kwenye Ghuba ya Guinea ya Atlantiki. Kabla ya kufikia Timbuktu (Niger) mto unapanuka kuwa na delta ya barani pia mdomo wake baharini pana delta kubwa sana.
Contents |
[edit] Historia
Njia ya pinde ya mto Niger ilichanganya wataalamu wa Ulaya pamoja na Waarabu kwa karne nyingi. Waroma wa kale walifahamu mto ule mkubwa karibu na Timbuktu wakafikiri ya kwamba inaendelea kujiunga na mto Nile. Mtaalamu Mwarabu Ibn Battuta alifikiri hivyo pia. Wengine waliona itaishia kwenye mto Senegal au mto Kongo. Kuchanganyikiwa huku kulisababisha kwa karne nyingi ramani zisizoonyesha mwendo halali wa mto. Wasafiri na wataalamu wa nje hawakuelewa ya kwamba mto mkubwa ulio karibu na Timbuktu na mto mkubwa unaoingia Atlantiki kwenye Ghuba ya Guinea huko Nigeria ni mto uleule. Ni tangu 1830 tu ya kwamba msafara wa kisayansi ulitambua hali halisi.
[edit] Tawimito
- Bani
- Sokoto
- Benue
- Béli
- Gorouol
- Tapoa