Guinea Mpya
From Wikipedia
Guinea Mpya kisiwa kikubwa katika Pasifiki upande wa kaskazini ya Australia. Ni kisiwa kikubwa cha pili duniani baada ya Greenland.
Eneo la kisiwa limegawiwa kati ya mataifa mawili:
- upande wa magharibi ni mikoa ya Indonesia ya Papua na Irian Jaya Magahribi.
- upande wa mashariki ni nchi huru ya Papua Guinea Mpya
[edit] Jiografia
Eneo lote la kisiwa ni 829,200 km² na jumla ya wakazi ni milioni 5.2 (2004).
Kuna milima mikubwa; upande wa Indonesia ni milima ya Maoke (Puncak Jaya 4,884 m juu ya UB) na upande wa Papua Guinea Mpya ni milima ya Bismarck (Mount Wilhelm 4,509 m juu ya UB). Mto mrefu kisiwa ni Fly.