Kihindi
From Wikipedia
Kihindi (Devanagari: हिन्दी au हिंदी) ni lugha ya kitaifa nchini Uhindi. Kinaeleweka kati ya theluthi mbili ya Wahindi wote yaani takriban watu milioni 650. Wasemaji wa Kihindi kama lugha ya kwanza ni zaidi ya milioni 180.
Kinahesabiwa kuwa kati ya lugha za Kihindi-Kiajemi ndani ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Lugha za karibu ni pamoja na Urdu, Kipunjabi, Kisindhi, Kigujarati, Kimarathi na Kibengali.
Lugha imetoka katika Sanskrit ya kale iliyokuwa lugha ya chanzo cha utamaduni wa Uhindi.
Makala hiyo kuhusu "Kihindi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Kihindi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |