Mawese
From Wikipedia
Mawese ni mafuta ya kulika kinachotolewa katika matunda ya miti ya mchikichi (Elaeis guineensis). Ni mafuta ya kupikia ya Afrika hasa penye asili ya mchikichi inayoitwa „Elaeis guenesis“ kutokana na kupatikana kwa wingi katika nchi za Guinea.
Contents |
[edit] Mawese kutokana na nyama ya tunda
Kuna aina mbili za mawese; mawese hasa hutolewa na nyama ya tunda ina rangi nyekundu na vitamini nyingi. Inatumika kama mafuta ya kupikia ama moja kwa moja ikitolewa na wakulima wenyewe na kuonyesha rangi nyekundu. Kama mawese inatengenezwa kibiashara kiwandani rangi inaondolewa kwa njia ya kusafisha mafuta kwenye vichujio. Baada ya kusafishwa huwekwa kwenye makopo au chupa na kuuzwa madukani au kupelekwa nje. Mafuta haya yanatumika pia viwandani kwa kutengeneza majarini, sabuni, mishumaa, mafuta ya kupakaa kwenye mwili na aina mbalimbali ya madawa na urembaji.
[edit] Diseli ya mawese
Mawese hutumika pia kiteknolojia na miaka ya nyuma kwa kutengeneza diseli. Hasa nchini Malaysia tekonolojia hii imesogea mbele. Malaysia inajaribu kupunguza gharama za kununua petroli na diseli kwa kutengeneza kiwanda kikubwa cha kusafisha mawese kuwa dieseli. Sheria ya Malaysia inadai kuanzia mwaka 2007 ya kwamba kila dieseli inayouzwa nchini iwe na 5% diseli ya mawese.
[edit] Mawese kutokana na kiini cha tunda
Aina ya pili ni mafuta yanayopatikana katika kiini cha tunda. Mafuta hii ina halijoto ya kuyeyuka kwenye 26 – 28 C°. Hivyo kwa kawaida ni ni imara si majimaji. Inatumika katika viwanda vya vyakula lakini pia kwa majarini. Intumika pia sana katika madawa ya urembaji na madawa ya kusafishia. Hata viwanda vya kutengeneza alumini hutumia aina hii ya mawese. Kuna biashara kubwa ya viini vya mchikichi kwa sababu husafirishwa bila kuharibu mafuta ndani yake.
[edit] Matatizo kutokana na matumizi makubwa
Nchi zinazopanda michikichi hasa ni Malaysia na Indonesia zenye mavuno ya 80% ya mawese duniani. Brazil na Kolumbia ziemanza vilevile kupanda michikichi kwa wingi. Uthai, Papua–Guinea Mpya na nchi za Afrika ya Magharibi zinachangia asilimia ndogo kwenye soko la dunia ya mawese. Kwa jumla mawese ina nafasi ya pili duniani kati ya mafuta kutokana na mimea inayotumika zaidi baada ya mafuta ya soya.
[edit] Mawese katika historia ya Afrika ya Magharibi
Mawese ilikuwa muhimu sana katika uchumi na historia ya Afrika ya Magharibi wakati wa karne ya 19 BK. Ulaya iliingia katika mapinduzi ya viwandani ikahitaji mafuta ya kutia grisi kwa ajili ya mashine za viwanda vyake. Mafuta haya yalipatikana katika nchi za Guinea hasa eneo la delta ya Niger.
Kiuchumi kwa nchi za Afrika ya Magharibi biashara ya mawese ilichukua nafasi ya biashara ya watumwa; hadi mwanzo wa karne ya 19 falme za pwani zilitajirika kwa kuwauzia wafanyabiashara wazungu watumwa kwa ajili ya masoko ya Amerika. Biashara hii ya watumwa ilipigwa marufuku polepole. Mabadiliko ya sheria katika Uingereza yalitangulia. Mapatano ya kimataifa kwenye Mkutano wa Vienna mwaka 1815 yalipakana biashara hii ikapungua hadi kwisha.
Umuhimu mpya ya Afrika ya Magharibi kwa ajili ya Ulaya ilikuwa mafuta ya mawese. Hasa viini vilipelekwa Ulaya kwa sababu mawese asilia huharibika haraka. Kabla ya kuwepo kwa viwanda Afrika penyewe viini viliweza kuisafirishwa mbali bila kuharibu mafuta ndani vyao. Mawese ya tunda lenyewe linaharibika kama haitengenezwi kwa kufuata mbinu mbalimbali zinazopatikana kiwandani lakini si rahisi kuzitumia katika uzalishaji wa kieneyeji.
[edit] Marejeo
[edit] Athari za kijamii na kiekolojia za matengenezo ya mawese
- Orangutan Film Protection Project
- Roundatable on Sustainable Palm Oil
- Friends of the Earth
- Website from the author of The Oil for Ape Scandal
- Palm Oil page from the Borneo Orangutan Survival Foundation